Rama Dee awachana wasanii hawa

Sunday , 13th Aug , 2017

Mkali wa R&B nchini Tanzania, Rama Dee amewataka wasanii kuacha tabia ya kujikweza na kuishi maisha ambayo siyo ya kwao kwa kuwa kufanya hivyo ipo siku itawagharimu katika utendaji kazi wao.

Msanii Rama Dee.

Rama Dee amebainisha hayo kupitia kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya kuwepo desturi ya baadhi ya watu wakiingia katika 'industry' ya muziki kukana maisha yake amabyo anayoishi kila siku na kujifanya yupo vizuri kila leo.

"Siyo lazima kujikweza maana ukijikweza ina kugharimu kwa sababu unaishi sehemu ambayo huwezi kukanyaga chini yani kwa hiyo ishi vile unavyoweza kuishi hata kama una chumba kimoja. Watu wanapaswa wawe wazi, usiogope shabiki yako kukuona wewe upo katika hali gani", alisema Rama Dee.

Kwa upande mwingine, Rama Dee amesema anajisikia furaha kwa sasa kuona watu wanajua kutofautisha muziki mzuri pamoja kiki.

Mtazame hapa Rama Dee anavyoendelea kufunguka