Jumapili , 9th Mei , 2021

Msanii Ommy Dimpoz yupo mjini Makka nchini Saudia Arabia, ameungana na waumini mbalimbali  wakiislamu duniani kufanya ibada ya Umrah baada ya mwaka 2019 kushindikana kutokana na kuumwa.

Msanii Ommy Dimpoz

Dimpoz amekuwa  ni mtu wa ibada siku zote na kupitia ukurasa wake wa Instagram, ame-post picha kadhaa akiwa ndani ya msikiti jirani “Al-Ka'abah” ambao ni nyumba maalum ya Mwenyezi Mungu na kawaida wahudhuriaji  huzunguka mara 7.

Makka ni mji mtakatifu wa Uislamu na kila mwaka mamilioni wa Waislamu wanahiji kwenda Makka.