Nilikuwa na wasiwasi mkubwa - Aslay

Wednesday , 11th Oct , 2017

Msanii Aslay Isihaka ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Natamba' amefunguka na kuweka wazi kuwa alikuwa na wasiwasi mkubwa kufanya kazi peke yake bila ya Meneja wake Mkubwa Fella na bila ya kuwa na uongozi wowote baada ya Yamoto Band.

Aslay amesama hayo alipokuwa kwenye kipindi cha Planet Bongo ya EATV na kudai kutokana na woga na wasiwasi huo ndipo hapo alipoamua kumtafuta meneja wake wa sasa Chambuso na kuanza kufanya kazi pamoja. 

"Nilikuwa na wasiwasi mkubwa sana kwamba tunaweza kusonga bila Mkubwa nyuma au menenjimenti yoyote baada ya hapo nikamtafuta Chambuso na yeye akaniambia kuwa tunaweza kusonga mbele, hivyo tupige kazi na kweli tukaanza kazi nakumbuka kazi yangu ya kwanza ilikuwa inaitwa 'Angekuona' hiyo niliachia kwenye TV na Radio mbalimbali, huo ndiyo wimbo ambao mimi unanigusa kutoka moyoni kwa sababu ni maisha yangu halisi kabisa" alisisitiza Aslay 

Mbali na hilo Aslay amesema kwa sasa bado hajapata mafanikio makubwa ila anaamini kuwa atapata mafanikio makubwa mbeleni na baadaye kuja kuwa kama wasanii wengine wakubwa ambao wananufaika vizuri kupitia muziki wao.