Nilianza kwa kuiba - Mr Blue

Friday , 13th Oct , 2017

Msanii wa Hip hop, Kheri Sameer Rajabu alimaarufu kama Mr Blue amefunguka na kusema kuwa yeye alianza muziki kwa kuiba 'verse' ya mtu kipindi alichokuwa mdogo na hivyo alipoimba na kupata shangwe sana kwa watu ndiyo kitu kilichomsukuma kufanya muziki

Mr Blue amesema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio ambapo leo alipewa Heshima ya Bongo fleva, Mr Blue amedai kuwa yeye alikuwa anaishi Kariakoo lakini nyumbani kwao kulitokea matatizo ya kifamilia hivyo alihama na kwenda kukaa Tandale na huko ndiko anadai kulikuwa chimbuko lake la muziki kwani watu aliowakuta huko walikuwa wanafanya muziki. 

"Kwa hiyo nilipohamia huko ndiko kulikuwa nyumba ya muziki, nikajikuta nawasikiliza sana na kukariri 'verse' hivyo kuna siku nilikwenda sehemu na kuchana verse ya mtu nilishangiliwa sana, kwa hiyo mimi naweza kusema nimeingia kwenye muziki kwa kuiba 'verse' ya mtu ambaye naye nilimkuta huko nilikohamia" alisema Mr Blue. 

Aidha Mr Blue amesema kuwa katika maisha yake ya muziki amekosa mengi ambayo alikuwa anastahili kuyapata kwenye muziki wake kama tuzo mbalimbali na jasho lake kwenye album zake alizotoa kipindi cha nyuma kwani hakunufaika nazo.

Itazame hapa video ya Mr Blue akimshukuru Mungu