Jumatatu , 19th Jun , 2017

Hit maker wa ngoma ya 'Quality Time', Nikki wa Pili amefunguka na kushauri kwamba  makampuni ya kigeni yanayopewa nafasi ya uwekezaji nchini yataifishwe ili kutoa nafasi kwa wazawa kuendelea na biashara hiyo ikiwa ni pamoja na kusaidia kutoa ajira.

Msanii Nikki wa Pili

Nikki amefunguka hayo ikiwa ni siku chache tangu  kupata nafasi ya kuhudhuria uwasilishwaji wa ripoti za  mchanga wa dhahabu (Makanikia) Ikulu, na kusema kwamba uwizi wa rasilimali haujaanza kufanyika leo hivyo ni vyema Serikali ikaachia sehemu nyeti kama madini wakapatiwa watanzania.

"Ripoti zote zimeshaonesha ni kwa jinsi gani tumeibiwa vya kutosha, hapa ningeishauri kwamba makampuni yote yanayosimamiwa na wageni kutoka nje yataifishwe na wazawa wakabidhile kuyaendeleza.  Wawekezaji wanakwepa kodi kwa kusaidiwa na viongozi  pamoja na wanasiasa wanaowapunguizia hizi kodi hivyo kwa namna moja au nyingine huu ni uwizi" - alisema Nikki

Nikki amezidi kwenda mbali kwa kutoa mifano kama "Kwa mfano sehemu kama Bulyanhulu kulikuwa na wachimbaji wadogo wadogo laki tatu amekuja muwekezaji mmoja wale wote wameondolewa walioajiriwa hawafiki hata elfu kumi hivyo ajira zaidi ya laki mbili imepotezwa, hii siyo tena uzalishaji wa ajira bali upokaji.  sasa hivi Arusha hakuna tena kina Papa King wapya kwa sababu ya wawekezaji walioingia migodini- Nikki aliongeza.