Nataka kubadili dunia – Diyen

Friday , 13th Oct , 2017

Msanii Diyen kutoka Rwanda ambaye anaishi Marekani, amesema muziki anaoufanya anataka ubadilishe dunia, kwa ujumbe atakao utoa.

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Radio, Diyen ambaye kwa sasa anasoma chuo cha muziki cha Full Sail nchini Marekani, amesema anataka kufundisha dunia kuhusu umoja na upendo kupitia muziki wake.

“ Nataka kufanya muziki ambao utafikia dunia nzima na kubadilisha kupitia mafundisho ya umoja na upendo nitakayoyatoa, nataka kukua zaidi na sitokata tamaa kwenye hilo”, amesema Diyen.

Diyen ambaye kwa sasa ana 'project na msanii mkubwa wa Nigeria, Wizkid, amesema anakabiliwa na changamoto kubwa za kufanya muziki akiwa nje ya Afrika Mashariki, ikiwemo kupata producers wanaojua midundo ya kiafrika.

“Kufanya muziki wa Kiafrika wakati naishi nje ni changamoto kubwa, kutafuta producers ambao wanaelewa ladha ya muziki wa Kiafrika ni shida sana huku, hata kutengeneza mashabiki ilikuwa ngumu lakini kwa sasa najitahidi kiasi chake.

Diyen ni msanii kutoka Rwanda, na kwa sasa anaishi Dallas Marekani kwa masomo.

Tazama hapa moja ya kazi zake