Jumatano , 14th Jul , 2021

Mwandishi wa nyimbo mbalimbali za wasanii wa Bongo Fleva akiwemo Nandy, Ommy Dimpoz, Maua Sama, Malkia Karen na wengine kibao, Logic amefunguka changamoto mbalimbali ambazo anazipitia wakati wa uandishi wa nyimbo na jinsi anavyonufaika na shughuli hiyo.

Picha ya Msanii Logic

Logic amesema kuwa biashara ya kuandikia wasanii nyimbo kwa Tanzania ni ngumu kutokana na wasanii hao kukataa kuingia mikataba ambayo itawafanya waandishi na wao wanufaike kutokana na mzunguko wa mauzo na matumizi ya wimbo husika.

Msikilize hapa akifunguka zaidi