Jumapili , 10th Mei , 2020

Kama ulifuatilia show ya Friday Night Live ya East Africa TV iliyoruka Mei 8,2020 utakuwa uliona ile vita ya maneno kati ya wanamitindo wawili ambao ni Calisah na Ben Breaker.

Mwanamitindo Calisah

Kufuatia tofauti zao zilimpelekea hadi Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Machezo Juliana Shonza kutoa neno kuhusu vijana kwamba tuheshimiane bila kujali nani mkubwa na nani mdogo ili kufikia malengo.

Muda mfupi uliopita kwenye ukurasa wa mtandao wa Instagram ambao anatumia mwanamitindo Calisah ameomba radhi kutokana na tukio za lugha alizoziongea kwenye interview hiyo.

"Najua wengi mmekwazika kwa majibu yangu mabaya na kupanik katika kipindi cha FNL ya #EATV kilichoruka juzi, nichukue fursa hii kuomba radhi kwa wale wote waliokwazika sikua nategemea, baada ya kutafakari kwa makini nikagundua kweli nilikosea" ameandiak

"Pili nichukue fursa hii kumpongeza kijana Mawenzangu Ben Breaker kwa juhudi kubwa anayofanya kwenye industry yetu na sisi wenyewe ndio wakushikana mikono, mwisho nashukuru mama yetu mlezi Juliana Shonza kwa ushauri wako mzuri juu ya sisi vijana, naahidi kutorudia tena na tutakua kitu kimoja, sanaa ni kazi na tuimarishe upendo" ameongeza