Jumatatu , 12th Jul , 2021

Msanii Dogo Janja amefunguka kusema msala anaoukumbuka kwenye maisha yake ya muziki ni siku aliyoenda kufanya show Tarime mkoani Mara baada ya shabiki kutaka kumuibia kofia na cheni alizovaa.

Picha ya msanii Dogo Janja

Dogo Janja anasema kipindi hicho alikuwa bado mdogo kiumri japo alishaachia Album yake ya kwanza na Tarime alienda kufanya show akiwa peke yake.

"Msala wangu ulikuwa Nyamongo Tarime kwenye show ilikuwa mwaka 2013, shabiki mmoja alikuwa anataka kuleta uhuni akapigwa ngumi nyingi mpaka akatoka nje,nilikuwa naimba jamaa akataka kuondoka na kofia na cheni, hiyo ndio ilikuwa mara ya kwanza kufanya show kule na sijaenda tena" ameeleza Dogo Janja

Dogo Janja ameongeza kusema hali hiyo ilimtisha na kumfanya kumwambia Promote aondoke usiku huo huo baada ya kumaliza show ili kurudi Dar es Salaam kwa kutumia usafiri wa Ndege.