Jumanne , 11th Mei , 2021

Rapa anayewakilisha pande za 'Dom Town' Mji Mkuu hapa nchini Tanzania, Dodoma Moni Centrozone ameshea orodha ya wasanii wake 10 anaowakubali kwenye upande wa muziki wa HipHop lakini cha ajabu hajamuweka mshkaji wake Country Wizzy.

Picha ya pamoja ya wasanii Country Wizzy kushoto, na Moni Centrozone kulia

Moni Centrozone ameeleza kwamba kwa bara la Africa anamkubali zaidi Jay Moe na dunia kwa ujumla anamkubali rapa J Cole.

Katika orodha yake hiyo ambayo ameiweka kwenye 'Insta Story' yake amewataja wasanii wafuatao 

1. J Cole 

2. Jay Moe 

3. Kendrick Lamar 

4. Nas 

5. Marehemu Albert Mangwea 

6. Marehemu BIG Notorious 

7. Jay Z 

8. Prof Jay 

9. Kanye West 

10. Post Malone