Mke wa Roma adai hawezi kurudia tena

Friday , 11th Aug , 2017

Baada ya kufanya kazi kubwa ya kumuwakilisha mume wake katika kutambulisha wimbo wake mpya 'Zimbabwe' Mke wa Roma Mkatoliki , Nancy amefunguka na kuweka wazi kwamba hii ndiyo itakuwa kazi yake wa kwanza na mwisho kwani hana kipaji cha kazi ya sanaa

Roma akiwa na mkewe Nancy anayemlisha Keki

Nancy amefunguka hayo wakati akifanya mahojiano na mwandishi wetu na kusema hana kipaji na uelewa mkubwa wa kazi za muziki lakini pia asingeweza kuacha kumsaidia mume wake katika kumuwakilisha kwenye vyombo vya habari ingawa ni kazi ambayo hadhani kama ataweza kuendelea nayo wakati mwingine.

"Siwezi kuendelea na hii kazi kwani mimi sina kipaji cha kazi hii kama usambazaji wa kazi hizi na idea ya muziki lakini kazi hii imekuja bahati mbaya na nimesimama kama muwakilishi na nimesimama kwenye hiyo nafasi" alisema Nancy

Aidha baada ya kuibuka maswali mengi kuhusu aina ya utambulishaji wa ngoma mpya ya msanii Roma Mkatoliki, Nancy amefunguka kwamba mumewe alishindwa kuacha kuachia wimbo huo kutokana na ukweli kwamba mume wake alishaweka maombi ya Interview kwenye vingi vya habari hivyo isingekuwa busara kutotokea. 

"Alishaomba interview kwenye vyombo vya habari kwamba hii wiki atakuwa na kazi mpya lakini akapata safari ya ghafla kwenda huko Zimbabwe na kwa sababu kuanza ku - cancell hizi interview ni kazi kubwa sana hivyo imenibidi mimi nibebe jukumu hili na kulisimamia ili yeye atakaporudi aendelee mimi nitakapoishia".

Aidha Mke wa Roma ameongeza kuwa "Mapokezi niliyoyapata ni tofauti na matarajio yangu kwani mimi sipo sana katika mambo ya muziki kwa sana lakini mapokezi ni makubwa sana na wimbo umeshaanza kufanya vizuri.

Bonyeza hapa kumsikiliza zaidi Nancy, Mke wa Roma