Alhamisi , 15th Jul , 2021

Mdau Miss Tanzania, MC mara tatu wa mashindano hayo na Mtangazaji wa kipindi cha Nirvana ya East Africa TV Deo amefunguka kuhusu sakata linaolendelea la Miss Tanzania Rose Manfere kuvuliwa taji la kutokwenda kuwakilisha mashindano ya Miss World.

Deo Kithama na Miss Tanzania Rose Manfere

Akizungumzia hilo kwenye sho wa DADAZ ya East Africa TV Deo ameeleza kuwa 

"Ukiwa Miss Tanzania kuna vitu unatakiwa kufanya vingine hutakiwi kwa mfano image yako kwenye jamii lazima iwe chanya vingine ni nidhamu na maadili, kama taasisi haijatoa tamko lolote ila leo mchana watataoa tamko"

"Miss Tanzania hajavuliwa taji ila taarifa iliyopo hatawakilisha mashindano ya Miss World, pia sio mjamzito labda ni masuala ya mkataba ndio taarifa nilizo nazo, ukiwa mrembo hutakiwi kuwa mjamzito au kuolewa ukiwa na taji".

Mengine zaidi tazama hapa kwenye video