Jumatano , 14th Jul , 2021

Miss Tanzania 2020/2021 Rose Manfere amefunguka kusema hana taarifa ya kuvuliwa taji la kwenda kuwakilisha nchi kwenye mashindano ya Miss World na badala yake atakwenda aliyeshika namba mbili kwenye mashindano ya Miss Tanzania

Picha ya Rose Manfere baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa Miss Tanzania

Akielezea hilo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram Rose Manfere ameandika kuwa.

"Nimeona kupitia mitandao kwamba mshindi namba mbili wa Miss Tanzania atawakilisha nchi kwenye mashindano ya Miss World, mimi kama Miss Tanzania 2020/21 sina taarifa rasmi, jambo lipo BASATA tusubiri taarifa, maamuzi na muongozo wa Baraza".