Alhamisi , 27th Feb , 2020

Msanii wa kizazi kipya Mo Music, amefunguka kuwa anapenda kuringa na anajisikia raha mashabiki wanapomuuliza kwanini harudi kwenye muziki, pia amesema mpaka Dunia inapinduka hakuna msanii atakayechukua nafasi yake.

Picha ya msanii Mo Music

Akipiga stori na eNewz ya East Africa TV, Mo Music amesema ameshakuwa staa na mtu mkubwa hivyo hawezi kushuka kimuziki.

"Tayari nimeshaacha alama na sijawahi kushuka kimuziki, mpaka Dunia inapinduka hakutakuwa na Mo Music mwingine, halafu mimi napenda kuringa na hakuna kitu kizuri kama shabiki anakuuliza kwanini haurudi, kwahiyo wanakuwa wanakumiss na una nafasi yako"  ameeleza Mo Music.

Pia ameendelea kusema kwa mwaka 2019 hakufanya chochote cha maana kwenye muziki kwa sababu alikuwa bize na biashara zake zingine, ambazo zilikuwa zinamsaidia kumuingizia pesa.