Ijumaa , 18th Jun , 2021

Rapper wa Marekani  XXXTentacion alipigwa risasi na kuuawa siku kama ya leo miaka 3 Iliyopita huko Florida katika tukio la shambulio nje kidogo ya RIVA Motorsports, duka la kuuzia pikipiki.

Picha ya msanii XXXTentacion

Washambuliaji hao walifanikiwa kukimbia na begi la Triple X ambalo lilikuwa na fedha muda mfupi baada ya kufanya tukio hilo la uhalifu. 

Kifo cha Triple X kilitokea Juni 18, 2018 akiwa na umri wa miaka 20 lakini hata hivyo washukiwa wanne wa tukio hilo walikamatwa.