Jumatatu , 10th Mei , 2021

Album ya "Game Over" ya mapacha kutoka Nigeria P-Square imefikisha miaka 14 tangu kuachiwa kwake mei,2007.

Wasanii wa kundi la P-Square

Album hii inatajwa kuwa na mafanikio makubwa sana ikiwa ni pamoja na kuuza zaidi ya nakala milioni 1 ndani ya wiki ya kwanza, zaidi ya nakala milioni 8 ulimwenguni kote rekodi ambayo ilidumu kwa muda mrefu na kushinda tuzo mablimbali.

Game over ilikuwa album ya tatu na ilibebwa na ngoma kali kama do me, no one like you, roll it, more than a friend na ifunanya.

Wimbo wa "No one like you" ulikaa namba moja kwenye chart mbalimbali kwa zaidi ya wiki nne.
Ripoti za juu ya kutengana kwao zilianza kuonekana baada ya Peter Okoye kuripotiwa kutuma barua ya kujiondoa kwa wakili wa kundi hilo,kabla ya kuvunjika mnamo 2016, ikidhaniwa juu ya kutokukubaliana juu ya utendaji wa meneja wao.