Jumanne , 13th Jul , 2021

The star kid wa BongoFlava Bright Music amesema Meja Kunta ndiyo mflame wa muziki kwa sasa licha ya kuwa na vichwa vingi vya muziki huo kama Msaga Sumu, Sholo Mwamba, Man Fongo na Mzee Bwax.

Kushoto ni Meja Kunta kulia ni Bright Music

"Ngoma yangu nimemshirikisha Meja Kunta, kwa sasa naweza nikasema Meja Kunta ndiye mfalme wa muziki wa Singeli, na nimeamua kufanya Singeli kwa sababu natafuta pesa, so popote kwenye pesa mimi naenda tu" amesema Bright Music 

Bright Music na Meja Kunta kwa sasa wameshirikiana kwenye wimbo mmoja unaoitwa 'demu wangu' na ngoma yao ipo trending namba 9 kwenye mtandao wa Youtube.