Jumatatu , 10th Mei , 2021

Kwa kipindi cha miaka ya 90’s mpaka 20’s ilikuwa ili msanii uweze kutoboa lazima ujiunge kwenye kundi lolote la muziki na ndio maana kwa kipindi hicho idadi ya makundi ilikuwa kubwa na yalidumu kwa muda mrefu tofauti na hivi sasa.

Pichani kushoto ni msanii Zavara, Professor Jay, Juma Nature na Crazy GK

Pia lengo kubwa lingine ilikuwa kuifanya Tanzania kuwa "Taifa la hip hop’’, kuondoa vijana kwenye maisha ya mtaani, hasa yale ya hali duni na kuweza kujitegemea. 

Haya ni baadhi makundi ya muziki ya bongo fleva ambayo yalifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuukuza muziki wetu na kuacha alama mpaka sasa.

1.Kwanza Unit (KU Creaw).

Kwanza Unit lilikuwa kundi la mwanzo kabisa la muziki wa hip hop na lilianzishwa mwaka 1990, liliundwa kutokana na muunganiko wa makundi matatu, KBC, Eazy-B, Fresh-G na D-Rob ni baadhi ya wasanii wa KUC.

Walifanikiwa kuachia kazi kama Real hip hop, Beyond belief remix, Acha na zingine kibao, awali walikuwa wana-rap kwa kiingereza lakini baadae walibadilika na kutumia Kiswahili.

2.Gangwe Mobb.

Temeke Mikoroshini ndiko maskani ya kundi hili yalipatikana na lilianzishwa mwishoni mwa miaka ya 90 punde baada ya Kwanza Unit, Mr. II na wengineo kuchangia muziki wa hip hop wa Kiswahili nchini kujipatia umaarufu, huku Inspector Haroun na Luteni Karama ndio walikuwa wanakikundi.

"Gangwe" walilenga hasa uhalisia wa hip hop ya watu wa mtaani na walitoa album kama Simulizi la Ufasaha, Nje ndani huku wakitamba na ngoma Ngangali, Mtoto wa Geti Kali nakdhalika.

3. Hard Blasters.

Ujumbe wao kupitia muziki ulibadilisha mtazamo wa jamii na kuamini kuwa kufanya muziki sio uhuni ni ajira/kazi.
Fanani, Crazy One, Professor Jay, KC1, Trigger F na Tuff Jam waliunda kundi hilo na waliachia album kadhaa “Funga kazi, Tuko nyuma kimaendeleo nakadhalika

4.Tmk Wanaume Family.

Ni moja ya kundi lililoleta mapinduzi makubwa kwenye muziki wa kizazi kipya tangu kuanzishwa kwake Septemba 16, 2002 mjini Mwanza, wakati wa uzinduzi wa album ya Juma Nature iitwayo Ugali na hadi sasa limejijengea umaarufu mkubwa kutokana na mtindo wao wa kucheza ujulikanao ‘Mapanga’.

Kabla halijavunjika lilikuwa na wasanii Juma Nature, KR, Doro, D Chief, Mh Temba, Mzimu, Luteni Karama, Chegge, Yp, Y Dash, na wengineo, halafu baada ya kutengana kukawa na "Tmk Wanaume Family" na Tmk Wanaume. Halisi” Wanaume kiongozi wa kundi alikuwa Mh Temba na Chegge wakati Tmk Wanaume Halisi kiongozi wa kundi alikuwa Juma Nature na Inspector Haroun, kwasasa wameungana tena.

5.Chemba Squard.

Hili ni miongoni mwa makundi yaliyokuwa na wasanii wenye vipaji na uwezo wa hali ya juu sana tangu walipoingia rasmi sokoni mwaka 2000, liliundwa na Noorah (Baba Stylz), Dark Master, The late Mez B na Mangwair na wote walikuta shule ya Sekondari Mazengo Dodoma.

Flow zao zilikuwa matata sana, walitisha kwenye kazi kama Party ya wana chemba.

6. East Coast Team.

Linaundwa na wasanii Ay, Mwana FA na Crazy GK ambao walifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuleta mabadiliko kwenye game kuwa ya kisasa zaidi, makazi yake ni Upanga mashariki.

Hii leo, Ama zangu, ama zao ni baadhi ya kazi zao zilizofanya vizuri sokoni.