Madee kumpiga Dogo Janja kwa hili

Saturday , 7th Oct , 2017

Msanii Madee Seneda ambaye pia ni kama baba kwa msanii Dogo Janja na meneja wake, amesema hachukizwi kwa skendo za Dogo Janja hususan za wanawake, kwani zinaonyesha uanaume wake, na iwapo ingekuwa kinyume chake angemchapa.

Akipiga stori na Grayson Gideon 'Back stage' kwenye Bongo Fleva Top 20 ya East Africa Radio, Madee amesema kitendo cha Dogo Janja kuwa na skendo za ngono ni kitu cha kawaida, na iwapo angesikia kinyume asingeweza kuvumilia na angemshushia kipigo.

Hivi karibuni Dogo Janja amekuwa na skendo za kujihusisha kwenye mahusiano ya kimapenzi na watu maarufu mbali mbali, akiwemo muigizaji wa filamu bongo Irene Uwoya na dada wa mjini Muna love, ambao wote ni wakubwa kiumri kwake.

Msikilize hapa Madee akifungukia suala hilo.