Jumatatu , 16th Mei , 2022

Kutoka familia maarufu ya Kardashian, inasemekana Kourtney na mwanamziki Travis Barker wamefunga ndoa nchini Italia.

Kourtney na Travis wakiwa nchini Italia

Taarifa kutoka TMZ, ndoa hiyo ilifungwa kimila na ilihusisha watu wachache wa karibu, katika picha zilizosambaa mtandaoni ndugu walionekana ni baba mzazi wa Travis pamoja na bibi yake Kourtney.

Oktoba mwaka jana Travis alimvalisha pete Kourtney katika fukwe za Montecito, California. Kabla ya mahusiano haya Kourtney alikuwa kwenye mahusiano na Scott Disick aliyedumu naye kwa miaka 10 na kufanikiwa kupata watoto watatu.