Jumanne , 13th Jul , 2021

Kupitia EATV & EA Radio Digital Baba Yaga Nay wa Mitego amefunguka kinachoendelea kati yake na Harmonize kwa kusema hana bifu na msanii huyo ila anashangaa ameblock kwenye mtandao wa Instagram.

Msanii Nay wa Mitego na Harmonize

Nay wa Mitego amesema yeye ni mtu ambaye hapindishipindishi maneno na kama ukikosea au ukimzingua atakuchana ukweli labda hiyo ndiyo sababu ya Harmonize kujishtukia na kumblock Instagram.

"Mimi sina tatizo na Harmonize, nipo straight sana hata kama ni mshkaji wangu ukinizingua au ukinikosea nitakwambia, pia ukifanya kitu cha ajabu nikahisi naweza kuzungumzia nitasema na usiponielewa unaweza ukanichukia, napenda kuzungumza kitu kilicho sawa

"Sijawahi kuwa na tatizo na Harmonize japokuwa nimeona ameniblock Instagram, ila nikifanya kitu changu ukajihisi basi kinakuhusu hata kama sitakutaja" ameeleza Nay wa Mitego

Mengine zaidi kuhusu Nay wa Mitego na Harmonize tazama hapo chini kwenye video.