Kendal Jener ameoneshwa kutofurahia mahusiano hayo baada ya kusema kuwa Tyga alitakiwa kuwa nyumbani na familia yake, kwa wakati ambao aliungana na familia ya Kardashian katika siku maalum ya mapumziko na familia ambapo familia hiyo ilienda kupumzika St. Barts.
Kwenye mfululizo wa kipindi chao cha Keeping up with the Kardashian dada yao mkubwa Kim Kardashian ambaye ni mke wa mwanamuziki maarufu duniani Kanye West, alisikika akiwataarifu kuwa Kylie anamleta Tyga kwenye safari yao, ndipo Kendal alipotoa maneno hayo.
“Ungechukua muda huu kuwa na familia yako”, alisema Kendal ambaye alikuwa anamwambia Kylie juu ya mpenzi wake Tyga.
Kylie na Tyga wameanza mahusiano yao mara baada ya Tyga kuachana na mpenzi wake Black Chyna, ambaye pia ni mama wa mtoto wake mmoja King, na kuibua minong'ono mingi kwa watu kuwa Kylie ndio chanzo cha kuachana na mama wa mtoto wake.


