Kajala avunja Ukimya, atoa tamko

Jumatatu , 7th Jun , 2021

Msanii wa filamu Kajala Masanja amevunja ukimya kwa kusema hajafikia hatua ya kukaa mikao isiyokuwa na maadili kama inavyosemekana kwenye baadhi ya picha iliyoeditiwa ikimuonesha yeye na mtoto wake.

Picha ya msanii wa filamu Kajala

Kajala amekanusha hilo kupitia page yake ya Instagram ambapo ametoa taarifa ndefu inayoelezea tukio hilo kwa kuandika kuwa,

"Kumekuwa na picha ikisambaa ikiwaonesha wanawake wawili wakiwa watupu kwenye mkao usiofaa na wanawake hao wameonekana wakitofautiana umri, picha hiyo ikaeditiwa na kuwekwa kichwa changu ama kinachofanana na changu huku watu wakisambaza kwa kusema ni mimi na mwanangu". 

"Hata kama nina ushenzi wa namna gani sijafikia na wala sitafikia huko hiyo ni laana iliyopitiliza sijui waliofanya hivyo wana malengo gani na mimi, sijawahi na sitawahi kupiga picha ya namna hiyo na binti niliyembeba tumboni miezi 9 na kumzaa kwa uchungu" ameongeza