Joh awafungukia 'Directors' Bongo

Friday , 19th May , 2017

Msanii wa ‘Hip hop’ Joh Makini mwenye 'hit song' ya 'Waya' amefunguka kwa kudai akiwa anafanya kazi na ma-director wa nje ya bongo anakuwa hana stress ya aina yoyote kwa kuwa anapata kila kitu 'on set' na 'very proffessional'.

Msanii wa ‘Hip hop’ Joh Makini

Joh ametoa kauli hiyo baada ya maswali ya watu wengi kutaka kujua ni kwanini anapenda kufanya kazi zake za muziki nje na kuwaacha watengenezaji wabongo wenye viwango vikubwa zaidi ya huko anapokwenda.

“Mimi siwezi kukuficha kwamba natafuta ubora, na 'standard' ambayo nime-set katika muziki wa Joh Makini, inanilazimisha kuendelea kwenda juu sio kurudi chini…Waongozaji wa bongo nawaamini sana lakini nakuwa 'comfortable' nikiwa nafanya video na ma-director wa nje mara nyingine kwa sababu nakuwa sina 'stress'....Napata kila kitu 'on set' na wao wanakuwa wanafanya kila kitu alafu 'very professional". Alisema Joh Makini

Pamoja na hayo Joh amesema endapo waongozaji wa bongo wataongeza kasi yao katika kuboresha video zao basi muda si mrefu wasanii nao wataachana na mfumo huo wa kwenda nje ya nchi kutafuta ma-director bali kama itawalazimu hivyo basi wataenda kwa lengo la kutafuta 'location' na vitu vya tofauti na bongo.