Alhamisi , 27th Mei , 2021

Ikiwa hata wiki moja haijafikisha album ‘Asante Mama’, Dogo Janja adata na kasi ya mauzo ambayo ameendelea kuyashuhudia ndani ya kipindi hicho kifupi.

Msanii Dogo Janja

 

Album hiyo yenye nyimbo 11 ikiwa ameshirikisha wasanii wakubwa wa kike bongo Mimi Mars, Nandy, Maua Sama, Khadija Kopa, Lulu Diva, Rosa Ree, Lady Jaydee na Linah mpaka sasa imepata streams zaidi ya laki 1 kwenye mtandao wa kupakua na kusilikilizia muziki Boomplay Music.

Janjaro amesema “Nimewahi kuamini katika upendo, sijawahi amini katika mkanganyiko,asanteni sana, inanipa hamasa zaidi ya kuendelea kufanya kazi nzuri’’.

Asante Mama ni album ya pili ya Janjaro na ilitoka Mei 21 mwaka huu.