Alhamisi , 12th Mei , 2022

Mshindi wa tuzo za Grammy mwanamziki J Cole amehudhuria mahafali ya shabiki wake ambaye alishawahi kumpa ahadi ataenda kwenye mahafali yake akifanikiwa kumaliza chuo kikuu.

J Cole akiwa na Cierra Bosarge.

Cierra Bosarge ambaye ni shabiki wa J Cole, alikutana na rapa huyo kwa mara ya kwanza mwaka 2013 baada ya kupiga simu kwenye Radio na kusema ndoto yake kubwa ni kukutana na J Cole katika siku yake ya kuzaliwa. Baada ya miezi mitatu akiwa shuleni alipigiwa simu na J Cole anahitaji kuonana nae.

Cierra alisoma bila malezi ya wazazi wake ambao walifungwa jela kwa matumizi ya madawa ya kulevya, na ndiyo kitu ambacho kilimshawishi J Cole kuwa karibu na binti huyo na kumpa ahadi ya kuhudhuria siku ya mahafali yake kwa niaba ya wazazi wake endapo atafanikiwa kumaliza chuo kikukuu.