Jumatano , 14th Jul , 2021

Ni Headlines za staa wa muziki Tanzania na Africa kwa ujumla Diamond Platnumz baada ya kutimiza ndoto zake kwa kununua gari la ndoto yake 'dream car' aina ya Rolls Royce ya rangi ya blue.

Msanii Diamond na gari yake mpya

Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram imeoneakana video ikimuonyesha Diamond Platnumz akilipokea gari hilo leo nyumbani kwake baada ya kushushwa kutoka kwenye Kontena.

Aidha mwezi mmoja uliopita staa huyo wa muziki alinunua gari mpya aina ya Cadillac Escalade Sky Captain inayodaiwa ina thamani ya Tsh Milioni 811.

Zaidi jionee hapa chini akishusha gari lake hilo.