Gabo Zigamba kabweteka - Duma

Sunday , 8th Oct , 2017

Msanii wa filamu za bongo Duma amefunguka na kusema kuwa msanii mwenzake wa filamu za bongo, Gabo Zigamba amebweteka kwani hakuna kazi anazofanya na kusema yeye hawezi kumuamsha mtu aliyelala.

Duma alisema hayo siku kadhaa zilizopita wakati akizindua filamu yake ya 'Bei kali' na kusema kuwa wao walimualika Gabo aweze kufika kwenye uzinduzi huo lakini msanii huyo ambaye ana mashabiki wengi nchini hakutokea. 

"Yeye kutokuwepo anakosa vitu vingi sana Gabo anashuka kimasoko, mimi na yeye hatuna mgogoro tunaelezana ukweli ili tuweze kuitoa tasnia hapa kuipeleka sehemu nyingine, mimi simkosei heshima sababu sijamtukana tusi hata moja Gabo anamashabiki wengi sana yeye amebetweka tu 'No man' fanya kazi" alisema Duma 

Mtazame hapa akifunguka mengi zaidi