Aliyeandika 'Komela' ya Dayna adai sifa zake

Friday , 21st Apr , 2017

Msanii chipukizi kwa sasa anyetamba na wimbo wa 'Star' Foby amekiri kukerwa na tabia ya msanii Dayna Nyange kushindwa kutambua mchango wake katika wimbo wa 'Komela' aliomshirikisha Billnass ambao unasumbua masikio ya watu kwa sasa.

Dayna (kushoto), na Foby

Kwenye story tatu ya Planet Bongo ya East Africa Radio Foby amedai kuwa wasanii wengi wamekuwa wakiwabania waandishi wa wimbo kwa kushindwa hata kutamka majina ya watu wanaoandika nyimbo zao.

Amewataka wasanii kubadilika na kuwataja hadharani watu waliowaandikia nyimbo zao huku akimtole mfano Dayna.

"Mimi nimemuandikia Dayna Komela imefanya vizuri sana lakini hajawahi kusema kama mimi ndo nimefanya kazi hiyo" Amesema Foby.

Pia amesimulia jinsi uandishi wa kazi hiyo ulivyomtea hadi usiku "Nakumbuka kazi yake niliifanya mpaka saa saba usiku, wakanishusha Afrikasana yeye na Billnass walikuwa wanaenda kwenye birthday party ya Nuh Mziwanda nikiwa nimeshamalizia kazi yake."

Foby pia amemtaja msanii mwingine ambaye aliuandikia ngoma na kushindwa kurudisha sifa "Pia Seline naye nimemuandikia naona hanitaji labda kwa sababu bado wimbo mpya huko mbeleni kama ataweza kunipa credit itapendeza sana, Sawa umenilipa lakini unaponitaja inanipa faraja zaidi. Uandishi ni biashara  unaponipa credit leo kesho unaniongezea wateja wengi" Amesema Foby