Enock Bella ataja kinachomtisha

Sunday , 16th Jul , 2017

Msanii wa muziki wa bongo fleva Enock Bella ambaye ni mmoja kati ya wasanii wanaounda kundi la Yamoto Band amefunguka na kusema muda wake kwenye muziki bado huku akidai saizi muziki unaushindani ambao hawezi kushindana nao akiwa mwenyewe. 

Msanii Enock Bella.

Enock Bella alisema hayo alipokuwa akihojiwa na eNewz na kusema kuna moja ya wimbo wake umevuja lakini yeye hawezi kuupa nguvu kwa kuwa hakuuachia yeye wimbo huo na kusema muziki wa sasa unahitaji mtu uwe umejipanga kwani ukifanya mchezo unaweza kupotea kabisaa kwenye ramani. 

"Kuna wimbo ulivuja lakini kwa kuwa mimi sikuutoa ilikuwa ni vigumu mimi kusimama nyuma ya wimbo huo na kuupa nguvu, mimi muda wangu wa kuachia wimbo na kutoka mwenyewe bado saizi angalia mwenyewe muziki jinsi ulivyokuwa na ushindani mkubwa, ukifanya kazi ili mradi iende utakuja kupotea mapema. japo saizi nipo na menejimenti lkini nategemea kupata uongozi uliomadhubuti ambayo nikikaa nayo nikianza kutoa kazi ni mpera mpera na si kurudi nyuma" alisema Enock Bella 

Mbali na hilo Enock Bella anasema management ambayo yupo nayo sasa bado hajasaini nayo mkataba wowote ule ila anafanya tathimini kuona jinsi gani hao watu wanaweza kufanya naye kazi, na jinsi gani anaweza kunufaika na uongozi huo.

  Mtazame hapa akifunguka zaidi 

Recent Posts

Mwanafunzi Aqulina Akwilini Baftaha aliyeuawa na poilisi

Current Affairs
CCM yatoa kauli yake kuhusu kifo cha mwanafunzi