Alhamisi , 5th Jan , 2023

Staa wa mziki nchini Diamond Platnumz ameweka wazi elimu aliyopewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) baada ya kuhudhuria Makao Makuu ya TRA siku ya jana Januari 4.

Picha ya Diamond na alama ya TRA

Diamond ameshea hilo kwenye ukurasa wake wa Instagram baada ya kuandika ujumbe ufuatao 

"Siku ya jana nilipata wasaa mzuri wa kuhudhuria Makao Makuu ya TRA, kuzungumza nao na Kupata elimu mbalimbali juu ya Kodi. kikao kilienda vyema na nikapewa elimu mbalimbali ambazo zitaongeza Ustawi bora wa kampuni na Biashara zetu, lakini pia namna sahihi ya kuendelea kuchangia pato la Taifa".

Zaidi bonyeza kutazama mazungumzo ya Diamond kuhusu elimu aliyoipata TRA.