
Msanii wa Muziki nchini Tanzania, Alikiba,
Akizungumza na EATV & EA Radio Digital, kuhusu kufanya ziara hiyo ya kimuziki mkoani humo Alikiba ameeleza kuwa.
"Tumejiaanda vizuri kama unavyojua, Iringa ni nyumbani Baba yangu ametokea huko na sisi ni wazawa wa huko, asili yetu ipo huko na ndugu zetu wengine wapo pia, kwahivyo tunakwenda sehemu ambayo tutafanya kitu maalumu na suprise zitakuwa nyingi na najivunia kwenda Iringa mwaka huu" amesema Alikiba.
Aidha ameendelea kusema ''Unajua sijafanya show Iringa kwa muda mrefu ila nimeamua kabisa kwenda kuwafanyia kitu hicho kwa sababu ya Unforgettable Alikiba".
Pia Alikiba ameumwagia sifa Mkoa wa Tabora, na kuwapongeza kwa heshima waliyompa alipofanya ziara hiyo mkoani humo, "Watu wa Tabora kama wanavyoona Asali ile ilivyokuwa tamu basi na wao wapo swadakta kabisa, sikuwahi kufika Tabora ila kwa mapokezi ambayo nimepata nimestahili kabisa na walinishangaza sana".