Jumatano , 18th Mei , 2022

Mwalimu wa mazoezi wa Alikiba Denzel Trainer amesema msanii huyo amemsafirisha kwa mara ya kwanza kwenda nje ya nchi South Africa kwa ajili ya kuongeza ujuzi kwenye kazi yake.

Picha ya Alikiba na Trainer wake Denzel

Akimzungumzia Alikiba kupitia Planet Bongo ya East Africa Radio Denzel amesema

"Mimi na Alikiba tumeanza kufanya kazi mwaka jana mwezi wa 9, akanisafirisha kunipeleka South Africa kwa ajili kumtrain yeye na kunipa ujuzi tofauti tofauti ili kuwa Trainer mkubwa kwake" 

"Ilibidi jana niende Kenya kuna chuo kule natakiwa nikakiangalie ili niendelee na mafunzo ya kukuza kazi yangu zaidi kwa muda wa wiki mbili. Mashavu yote hayo kwa ajili ya Alikiba, namshukuru sana".

Zaidi tazama hapa kwenye video.