Ijumaa , 8th Oct , 2021

Hitmaker wa Bongo Fleva, Kayumba ameonyesha nia na matamanio ya kutaka kufanya kazi ya pamoja (collabo) na kaka zake kwenye game ambao ni Mwana FA,  AY na Ommy Dimpoz.

Picha ya wasanii wa Bongo Fleva AY (kushoto), Mwana FA (katikati) na Kayumba

Kayumba amefunguka hilo kupitia ukurasa wake wa instagram baada ya ku-post picha na wakali hao wa Bongo Fleva walizopiga kwenye siku ya usikilizwaji wa albamu mpya ya Alikiba 'Only One King' na kuambatanisha ujumbe wenye matamanio ya  kufanya chorus kwenye wimbo utakaowakutanisha pamoja.