
Msanii mkongwe wa BongoFleva 20 Percent
Akipiga stori na Big Chawa kwenye kipindi cha PlanetBongo ya East Africa Radio, msanii huyo ameeleza kuwa, "Ile ngoma ya Mama Neema ni stori ya ukweli japo hainuhusu mimi moja kwa moja na ilitoka mwaka 2007, Neema sasa hivi ni mkubwa na anajiheshimu pia anasifa kama za Monalisa japo kwa sasa yupo nchini Rwanda, halafu binafsi nimebarikiwa kupata watoto wa kutosha yaani ninao wengi" amesema 20 Percent.
"Nakuja na filamu ya pili ya Mama Neema, itaonesha Neema alivyotoroshwa na mama yake mdogo kwenda Rwanda, kipindi naiachia ile filamu zilivumishwa stori eti nilikataza nyimbo zangu zisipigwe kwenye Media, ndiyo maana nikazihamishia kwenye ile filamu" ameongeza.