Jumatano , 16th Mei , 2018

Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Fabian Dakaro, amesema Serikali haitasita kuwachukulia hatua wafanyabiashara watakaouza sukari kwa bei ya shilingi 2600 kwa kilo au shilingi 3000 kwani watakua wanahujumu wananchi.

Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Arusha, Dakaro amesema wamepokea malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu kupanda kwa bei ya sukari pamoja na kubaini tatizo hilo wakati wa kufanya msako na mahala kwa wafanyabiashara wa bidhaa hiyo.

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya amesema kuwa Sukari iliyo katika vifungashio bei yake pia isizidi 2600 kwa kilo huku akisema kuwa usimamizi wa bei ya sukari mkoani humo ni endelevu na unapaswa kufanyika kwa kushirikiana na viongozi wa kata na vyombo vya dola.

"Nimeagiza Watendaji wa Kata wakasaidane na watendaji wa mitaa . Hili zoezi ni endelevu. Tutaendelea pia kufanya ukaguzi kwenye  maghala. Sukari za kwenye vifungashio tutaweka bei ambayo hatazi hata 2800 kwa hapa mjini," Daqqaro