Miili 12 yaopolewa majini Ziwa Victoria

Monday , 9th Oct , 2017

Miili ya watu 12 imeopolewa hadi sasa katika tukio la kuzama kwa gari aina ya Hiace katika Ziwa Victoria Mwanza, watu hao walikuwa ndani ya gari hiyo ambayo ilikuwa imebebwa na kivuko kilichokuwa kinatoka Mwanza kwenda Sengerema.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa mpaka sasa waokoaji wamefanikiwa kuokoa watu watatu na kuopoa miili ya watu 12 waliokuwa ndani ya gari hilo  ambalo limetumbukia ziwani baada ya kuteleza kwenye kivuko. 

Wakoaji hao wamefanikiwa kulitoa gari hilo aina ya Hiace ambalo lilizama ziwani ambapo watu 12  wamefariki dunia huku wengine watatu wakiwa wameokolewa wakiwa na majeraha mbalimbali mwilini.   

Gari hiyo aina ya Hiace lililtumbukia ndani ya Ziwa Victoria, eneo la Kigongo Feri wilayani Misungwi na kusababisha vifo watu 12 na majeruhi watatu.