Waziri adai wanaume hawaonekani hadi utumie miwani

Jumatano , 16th Jun , 2021

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima, amesema kuwa wanaume hawapo na kuonekana kwao ni hadi uwatazame kwa kutumia miwani ya X-ray.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima.

Kauli hiyo ameitoa leo Juni 16, 2021, Bungeni Dodoma, mara baada ya Mwenyekiti wa Bunge Mh. Mussa Azzan Zungu, alipomuita kwa ajili ya kujibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Viti Maalum, Mh. Halima Mdee, ambapo Mh. Zungu aliuliza kwamba 'Wanaume mpo?".

"Mheshimiwa Zungu wanaume hawapo, inakuwa shida sana kuwaona mpaka uvae miwani ya X-ray," alijibu Waziri Dkt. Gwajima.