Jumatano , 17th Nov , 2021

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ameendelea kutoa wito kwa wawekezaji kuja kuwekeza nchini kwa sababu Tanzania ina ardhi, barabara na umeme wa kutosha.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Aidha, Waziri Majaliwa pia ameiagiza Wizara ya Viwanda na Biashara kuendelea na utaratibu wa kukutana na wizara au taasisi za serikali na binafsi nchini ili kuwahamasisha kununua bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.

"Wawekezaji njooni muwekeze Tanzania, tuna ardhi ya kutosha, umeme, barabara, tuna reli ya kati na tunajenga reli ya kisasa, pia tuna ndege 11 na nyingine zinakuja, tunajenga viwanja ya ndege kila mkoa, hivyo tunauhakika wa usafiri," amesema Waziri Mkuu.

Kadhalika, Waziri Mkuu ametoa wito kwa wafanyakazi wa viwanda hapa nchini  kuwasaidia wawekezaji hao ili wakuze zaidi biashara zao na wanufaike na uwekezaji huo.