Jumatano , 18th Mei , 2022

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema watoto zaidi ya Milioni 10 wanatarajiwa kupata chanjo ya Polio nchini Tanzania

Waziri Ummy pia ameagiza vyombo vya usalama kuwachukulia hatua watu wanaosambaza taarifa za uongo na upotoshaji kuhusu chanjo ya Polio inayotolewa nchini.

Waziri Ummy amebainisha hayo leo Jijini Dodoma kwenye uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya utoaji wa chanjo ya matone ya ugonjwa wa Polio ambapo amesema taarifa hizo za  za uongo na upotoshaji zina lengo la kuzorotesha utoaji wa chanjo nchini.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka amewataka wazazi na wananchi wa mkoa huo kuwa mstari wa mbele kufanikisha kampeni hiyo ili kuokoa maisha ya watoto.