Alhamisi , 18th Aug , 2022

Watu watatu wa familia moja wakazi wa kitongoji cha Idoselo kijiji cha Kasesa kata ya Kaseme mkoani Geita wamefariki baada ya kupigwa na Radi iliyoambatana na mvua 

Watu hao ni Mageni Nkoma (70) Melisiana Ludeba (56)na Kelvin Shedrack mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi 9 

Wakizungimzia tukio hilo ndugu wa familia wanaelezea jinsi ambavyo mvua kali iliyoambatana na Radi ilivyochukua uhai wa wanafamilia wemzao

Diwani na mbunge wa jimbo hilo wamewataka wananchi kuchukua tahadhari juu ya mvua ambazo zimekuwa zikiendelea ili kuepukana na madhara yanayosababisha kupoteza maisha