Jumatano , 30th Nov , 2022

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera ameliagiza Jeshi la Polisi kutoa mafunzo kwa wamiliki wa silaha ili kupunguza wimbi la watu wanaojichukulia sheria mkononi na kugharimu maisha yao na watu wengine

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera ametoa maagizo hayo wakati anazungumza na wanahabari kuhusu ongezeko la vitendo vya ukatili ikiwemo mauaji

Aidha Homera amesema katika kuhakikisha wanadhibiti vitendo vya uhalifu mkoani Mbeya, tayari wamekamata watu watatu kwa tuhuma za kughushi  hati  mbalimbali zikiwemo za kumiliki ardhi.