Jumatatu , 26th Sep , 2022

Serikali imeagiza kukamatwa na kufikishwa mahakamani watu wote watakaobainika kuharibu vyanzo vya maji, ikiwamo miradi ya maji safi na salama inayojengwa vijijini kwa lengo la kuondoa adha ya wananchi kutembea umbali mrefu, kwenda kutafuta huduma hiyo nyakati za usiku 

EATV ilifika katika shughuli ya mazishi ya vijana hao na hapa mkuu wa wilaya ya Geita Wilson Shimo anakemea wachimbaji kuacha kuvamia maeneo yaliyofungiwa ili kulinda maisha yao

"Tusifanye njia ambazo ni haramu za mkato mkato, kama ambazo ndugu zetu hawa walifanya, ni ajali ndio kweli ni ajali, lakini inapotokea inapofanyika kwenye eneo ambalo sio sahihi kwa muda ule mahali pale, tunasema hata hivi vifo havikuwa sahihi, tutaendelea kuzika vijana wangapi, wanaofukiwa na mchanga au udongo machimboni, mara kwa mara kwenye duara ambazo si salama kuzichimba, tufanyeni machimbo katika maeneo ambayo ni sahihi, rasmi na tufanye kwenye muda na masaa ambayo ni sahihi pia",alisema Shimo.

Kaimu Afisa Madini mkoa wa Geita Dotto Ernest anasema Mgodi huo ulishafungiwa kutokana an sababu za kiusalama lakini wachimbaji wadogo wamekuwa wakienda kinyemela kuchimba usiku wa manane.

"Tujifunze kufanya kazi chini ya maelekezo ya ofisi ya tume ya madini kwa ujumla kwa eneo lile lilikuwa halifanyiwi kazi, wenye maduara walikuwa nayo pale yakajaa maji wakayatelekeza, hiyo ndio taarifa kamili ambayo ipo ofisini sasa wenzetu kwa bahati mbaya wakajikuta wanaenda kufanya kazi kwenye eneo lile", alisema Ernest.
Baadhi ya wachimbaji waliofanya uokozi wa miili ya wenzao wanaelezea tukio hilo.

"Walifukiwa wakiwa wanachimba, sababu walipigwa kwa ndani katika maeneo hayo sanasana wanachimba sio kama walikuwa juu ya maduara, hapana walikuwa ndani ya duara", alisema Manyandodi.

"Tukio hili lilitukuta yalikuwa majira ya saa11 za kuelekea asubuhi, nilifika kweli nikakuta tukio nililoambiwa la kupondwa vijana hao wa Sobola badae pale tukafanya jitihada za kuweza kuwaokoa lakini ilikuwa ni kazi  kifusi kilichokuwa kimemwagiwa kwa ndani kilikuwa ni kikubwa, watu waliitikia kweli tukaanza nao kufanya kazi za uokozi, baadae tulipomaliza kufanya kazi za ufukuzi tukawapata marehemu tayari walishapondwa, wamesgafariki na tukawatoa pale nje", alisema Kisinza.