Wananchi wapinga ujenzi wa kiwanda

Sunday , 16th Jul , 2017

Wakazi wa maeneo ya Mjimwema kata ya Malangali kwenye manispaa ya Sumbawanga, wamepinga vikali ujenzi unaoendelea wa kiwanda cha kusindika nafaka, jirani kabisa na Zahanati ya Malangali hali itakayoathiri utendaji wa zahanati hiyo na afya za wagonjwa

Wananchi hao wa kata hiyo wakiongea mbele ya mbunge wa Sumbawanga mjini Mheshimiwa Aeshi Hilal, wamesema kiwanda hicho cha kusindika nafaka kikianza kufanya kazi, kitaathiri mno hali za wagonjwa wanaopata huduma kwenye zahanati hiyo, ikiwa pamoja na akina mama wajawazito wanaotegemea kujifungua katika zahanati hiyo.

Kutokana na hali hiyo wananchi hao wamepinga vikali ujenzi wa kiwanda hicho na kusema haupaswi kuendelea katika eneo hilo 

Akizungumza na wananchi hao mbunge wa Sumbawanga mjini Mheshimiwa Aeshi Hilal, amesema licha ya serikali ya awamu ya tano kuhimiza ujenzi wa viwanda nchini, lakini ujenzi huo ni lazima uzingatie sheria na taratibu zote za afya na mazingira kwa ujumla, na hasa ikizingatiwa kuwa manispaa hiyo imeshatenga tayari maeneo ya uendelezaji wa viwanda.

Recent Posts

Mwanafunzi Aqulina Akwilini Baftaha aliyeuawa na poilisi

Current Affairs
CCM yatoa kauli yake kuhusu kifo cha mwanafunzi