Tamko hilo limetolewa leo na Mkurugenzi wa bodi hiyo bwana Jerry Msabi alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kwamba , wanafunzi ambao hawata tekeleza agizo hilo awatapata mkopo mwingine na watatakiwa kurudisha kiasi cha pesa ambacho walikwisha pewa na bodi hiyo.
Mkurugenzi huyo amesema, uhakiki huo utaisaidia serikali kubaini uwepo wa wanafunzi wasio stahili kupata mkopo na kutoa fursa stahiki kwa wale wanaotakiwa kupata mkopo huo ambapo amesema taasisi kumi na nane uhakikiwao tayari umekamilika.
Aidha Sabi amesema, mpaka sasa zaidi ya wanafunzi 2000 awajajitokeza kuhakiki taarifa zao na kutoa wito kwa wanafunzi na taasisi mbalimbali za elimu ya juu kutumia muda wa siku 7 uliotolewa na bodi hiyo kuhakiki taarifa zao na kuingizwa kwenye orodha mpya ya malipo
Agizo la uhakiki wa taarifa ya orodha ya majina ya wanafunzi wanaopokea mkopo wa elimu ya juu nchini ilitolewa na wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kwa lengo la kutambua endapo kuna wanafunzi hewa na wasio stahili kupewa mikopo hiyo.





