Alhamisi , 15th Jul , 2021

Wajawazito na wagonjwa wanaoenda kupata huduma ya afya katika Zahanati ya Kakese wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi, wamekuwa wakinyanyaswa na kupewa adhabu za kufanya usafi na kubeba tofali kichwani na watumishi wa hospitali hiyo bila kuwa na kosa lolote.

Matofali

Kero hiyo pia imetolewa na wakazi wa Kata hiyo hasa wanaume, jambo linalowaumiza zaidi pindi wake zao wanapoenda kliniki kujua maendeleo ya afya zao, badala ya kuwapa huduma za kitabibu wanawapa adhabu za kufagia na kusomba tofali.

Akijibu malalamiko ya wananchi hao Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu, amewataka wahudumu wa afya wa kituo hicho kuzingatia maadili ya kazi yao na kuacha mara moja tabia ya kuwafanyisha kazi wagonjwa na kuwanyanyasa.