Jumanne , 6th Jul , 2021

Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum, amesema kuwa katika dini ya Uislamu kuvishana pete kwa wachumba si utamaduni wa dini hiyo na badala yake jambo lililojema ni kwa wazazi kutaja mahari nyepesi na si kugeuza mahari kama biashara.

Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum

Kauli hiyo ameitoa leo Julai 6, 2021, kwenye kipindi cha SupaBreakfast MenuMpya, na kuongeza kuwa katika Dini ya Uislamu pia uchumba hautakiwi kukaa muda mrefu ili kuepusha husda na maneno ya watu yanayoweza kupelekea jambo hilo lisitimie.

"Kwetu sisi waislamu kuvishana pete si tamaduni yetu, jambo lenye kupendeza ni mahari kuwa nyepesi, ikiwa wazazi wanatumia watoto wao kama biashara kwenye suala la mahari au wanachelewesha posa wakiwa na sababu zao ambazo si za msingi hilo jambo halikubaliki," amesema Sheikh Alhad.