Alhamisi , 24th Mei , 2018

Afisa Uhamiaji mkoa wa DSM,Chrispine Ngonyani amebainisha raia kutoka nchi ya Ethiopia wamekuwa wakiwasumbua idara ya uhamiaji nchini kwani kila mara wanapokamatwa wahamiaji haramu wao huwa ni wengi zaidi.

Bw. Ngonyani amezungumza hayo wakati akitoa taarifa za utendaji kazi wa idara hiyo kwa wanahabari ambapo amesema kuwa tatizo la raia kutoka Ethiopia siyo  tu kwa uhamiaji Dar es salaam bali nchi nzima wanakumbana nalo.

"Raia wa Ethiopia wanatusumbua sana yaani kila tukikamata watuhumiwa kwa wingi, basi unakuta ni waethiopia ambao hawapungui 50 hadi 80 hilo ndo kundi la watu wanaotusumbua sana Idara ya Uhamiaji mkoa wa Dar es salaam" amesema.

Pamoja na hayo Bw. Ngonyani ameeleza kuwa idara hiyo kwa kipindi cha mwezi Januari 2018 hadi Mei 24, 2018 wameafanikiwa na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa 602 ambapo kari yao watuhumiwa 227 walikuwa raia wa Ethiopia na kati ya mashauri 118 yaliyofunguliwa Mahakama ya Kisutu raia wa Ethiopia walikuwa 214 na kati ya mashauri yaliyomalizika yalikua 99 na kati ya watuhumiwa 341 raia wa Ethiopia walikuwa 218.

Mbali na hayo Afisa huyo amesema Idara imefanikiwa kuingiza faini ya shilingi Milioni 121.5 na kati watuhumiwa waliofungwa ni 187 na mashauri yanayoendelea mahakamani ni 73 huku raia 28 wakupewa oda ya kurudishwa kwao.