Alhamisi , 11th Aug , 2022

RC Rukwa Queen Sendiga, amesema anatamani kuona mkoa wa Rukwa ukifanya mapinduzi makubwa katika sekta ya kilimo ili kiwe cha kibiashara na kukuza uchumi wa wananchi na kuwataka wataalam wa kilimo kuja na mikakati ya kufanya kilimo kikuze pato la wananchi na kuongeza uhakika wa chakula.

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Queen Sendiga

Mkuu huyo wa mkoa amesema hayo wakati wa hafla rasmi ya makabidhiano ya ofisi toka kwa mtangulizi wake Joseph Mkirikiti kufuatia Rais Samia Suluhu Hassan kumteua kuwa mkuu wa mkoa huo.

"Natamani kuiona Rukwa ikifanya mapinduzi makubwa katika kilimo, maafisa kilimo na ugani jitahidini kuwa na mipango mizuri ili kilimo chetu kiwe cha kibiashara na kuhusisha vijana wengi," amesema Sendiga.

RC Sendiga meongeza kuwa mkoa lazima uwe na mkakati wa kufanya vijana wengi kurudi vijijini ili kufanya kazi za kilimo hatua itakayowapatia uhakika wa ajira hivyo kutimiza lengo la Rais Samia kutaka kuona kilimo kuzalisha ajira nyingi nchini.