Ijumaa , 9th Dec , 2022

Vijana nchini wameshauriwa kufahamu kwamba viongozi waasisi wa Taifa la Tanzania walifanya kazi kubwa ya kuhakikisha Uhuru unapatikana hivyo  na wao wanao wajibu wa kuitunza na kuilinda amani iliyopo ili isitoweke

Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Elihuruma Mabelya,

Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Elihuruma Mabelya, wakati wa mdahalo wa miaka 61 ya Uhuru wa Tanganyika uliofanyika katika chuo kikuu kushiriki cha elimu Dar es Salaam (DUCE).

Kwa upande wao wahadhiri wa chuo hicho wameeleza miaka 61 ya Uhuru wa Tanganyika kwa jinsi ulivyofanikisha kukuza kiwango cha elimu hapa nchini na kuongeza idadi kubwa ya watalaam wa fani mbalimbali ambao wameisaidia serikali kuokoa fedha nyingi za kwenda kuwatafuta watalaam hao nje ya nchi.

Nae Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Amani wilaya ya Temeke Mchungaji Andrew Mtweve, amesema miaka 61 ya Uhuru wa Tanganyika imekuwa na uhuru mkubwa wa kuabudu kwa viongozi wa dini zote kukaa pamoja na kuzungumza huku makundi ya watu wenye ulemavu yakieleza kwamba bado  makundi hayo yamekuwa yakiachwa  nyuma kwenye masuala ya kiuwakilishi.